Jeshi la Uganda lafutilia mbali maandamano ya upinzani
Imechapishwa:
Jeshi la Polisi nchini Uganda limefutilia mbali maandamano ya upinzani ambayo yalipagwa kufanyika siku Ijumaa kuunga mkono mapinduzi ambayo yamefanyika katika mataifa yaliyopo Kaskazini Mwa Bara la Afrika.
Matangazo ya kibiashara
Kamanda wa Polisi wa Mji Mkuu Kampala Andrew Kiweesi amesema iwapo wapinzani hao watakaidia mari ya kufutwa kwa maandamano hayo basi watakuwa tayari kutumia nguvu kuwasambaratisha wote.
Kamanda Kiweesi ameweka bayana eneo ambalo lilipangwa kwa ajili ya maandamano hayo litakuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ili kudhibiti mtu yoyote asiweze kuingia eneo hilo kwa kesho.