Libya

Amnesty Inrernational laitaka baraza la mpito nchini Libya kuzuia ukikwaji wa haki za binadamu

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limesema kuwa baraza la mpito la Libya limesema wapiganji wa Libya wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, hivyo barza hilo latakiwa kuchukuwa hatua madhubuti kuzuia ukiukaji huo wa haki za binadamu unaofanywa na wapiganaji wanaompinga Gaddafi kuendelea.

Matangazo ya kibiashara

Hayo ni kwa mujibu wa utafiti wa repoti iliotolewa na shirika hilo la kutetea haki za binadamu.Imesema mashambulio ya vikosi vya Gaddafi kwa waandamanaji wa kiraia yalikuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati kukamatwa ovyo kwa watu na kuteswa kwa wafungwa ulikuwa ni uhalifu wa kivita.

Shirika huilo pia limewalaumu waasi kwa kuhusika na vitendo hivyo na kuonya kwamba kuanguka kwa Gaddafi kumesababisha kuwepo kwa ombwe la usalama nchini humo ambapo waasi wameitumia hali hiyo kwa kulipiza visasi na kufanya utesaji. Repoti hiyo imezingatia uchunguzi uliofanywa na watafiti walioitembelea nchi hiyo wakati uasi ulipoanza hapo mwezi wa Februari na mwishoni mwa mwezi wa Julai.

Mapema, Muammar Gaddafi alisisitiza katika ujumbe kupitia televisheni kuwa wataendelea na mapigano hadi "wapate ushindi".

Kwa sasa haijulikani kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69 yuko wapi.