Gambia-Guinea

Gambia yakanusha kuhusika katika jaribio la kummalizia maisha rais wa Guinea

Wikimedia Commons

Serikali ya Gambia imekana kuhusika katika jaribio la mauaji ya rais wa Guinea Alpha Conde mwezi julai kufuatia rais huyo kushutumu Senegal na Gambia kwa kujihusisha kwao na jaribio hilo.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Gambia imesema kuwa haijahusika na mipango ya kumuua rais wa Guinea na kusisitiza kuwa hawatazichukulia shutma hizi juujuu.

Wizara hiyo imemtaka Konde kutotoa shutma zisizo na msingi dhidi ya Gambia
Akiwa katika mahojianao na kituo cha redio cha nchini Senegal, Alpha Conde alisema kuwa shambulio la roketi katika makazi yake lilipangwa mjini Dakar na anashuku serikali hizo mbili zilijua mpango huo.

Nayo wizara ya mambo ya nje ya Senegal imesema shutma hizo zimeishtua nchi hiyo na kukana kutohusika katika shambulio hilo na kujitetea kuwa siku zote Senegal imekuwa ikiwakaribisha wanasiasa wa nchini Ginea akiwemo Konde.