Kenya-Nairobi

Idadi ya watu waliouawa nchini Kenya yazidi kuongezeka

Waokozi wakisaidia watu baada ya Bomba kulipuka mjini Nairobi
Waokozi wakisaidia watu baada ya Bomba kulipuka mjini Nairobi Vill

Idadi ya watu waliouawa jana mjini Nairobi katika mtaa wa Sinai Lunga Lunga jijini Nairobi nchini Kenya, yazidi kuongezeka. Duru za serikali zaarifu kuwa inaelekea watu 120 wanahofiwa kuaga dunia baada ya kuchomwa moto, wakati bomba la mafuta lilikupasuka mchana wa jana. Inaelezwa kuwa huenda idadi hiyo ikaongeza zaidi ,kwani hadi sasa jitihada zinaendelea kutafuta miili zaidi na manusura.

Matangazo ya kibiashara

Duru nyingine zinaarifu kuwa zaidi ya watu mia moja ndio ambao wamekufa baada ya bomba la mafuta kupasuka na kulipuka katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Mlipuko huo umetokea katika eneo la viwandani la Lunga Lunga na askari wa zima moto walipambana na moto mkali ambao ulikuwa ukitishia makazi ya watu mjini humo.

Bomba hilo la mafuta limepita katika makazi ya watu wengi kwenye mitaa ya mabanda katikati ya mji wa Nairobi na Uwanja wa ndege.

Zaidi ya majeruhi 100 wamepelekwa hospitali.

Msemaji wa magari ya huduma za dharura alisema waathirika wengi waliungua kiasi cha kutotambulika.

Taarifa zinasema mlipuko huo huenda umesababishwa na kishungi cha sigara kilichotupwa katika mtaro wa maji ambao ulikuwa ukielea mafuta.

Polisi na jeshi wameweka vizuizi katika eneo hilo, ambapo wakazi walisema kuvuja kwa mafuta kwenye bomba hilo na kusababisha watu wengi kukimbilia kuchota mafuta yaliyovuja.