Sudani

Sudani imeridhia kufanyika kwa operesheni ya kijeshi katika jimbo la Blue Nile

Rais wa Sudan, Omar el-Béchir akipeperusha mkono wa salam kwa wanajeshi  walio Kordofan
Rais wa Sudan, Omar el-Béchir akipeperusha mkono wa salam kwa wanajeshi walio Kordofan REUTERS/ Stringer

Sudan imeridhia kufanyika kwa operesheni ya kijeshi katika eneo la jimbo la Blue Nile lililo mpaka na Sudani kusini zikiwa ni siku kadhaa baada ya pande mbili hasimu kukubaliana kuondoa vikosi katika eneo jingine la mpaka kati ya sudan na sudani kusini.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa kamati inayojihusisha na maswala ya dharura, Ismail al-Haj Mussa amesema
bunge la nchi hiyo limeridhia kufanyika operesheni hiyo katika jimbo la blue nile ,eneo ambalo limekuwa likiwa na uhusiano na makundi ya waasi.

Akiongea na Bunge mjini Khartoum Mussa amesisitiza kutotaka taifa la Sudan kuingiliwa na kuwekewa mashinikizo na mataifa ya kigeni kwa kuwa Sudan imeamua kuendelea kutekeleza maamuzi yake.

Hatua hii mpya imekuja baada ya serikali mbili za Sudani na Sudani kusini waliweka makubaliano wiki iliyopita kuondoa vikosi vyao kutoka mpaka wa mji wa Abyei eneo ambalo vikosi vinavyooangalia usalama kutoka umoja wa mataifa vikiendelea na operesheni yake.