Syria

Shinikizo zaidi laongezeka kumtaka rais wa Syria kuachia ngazi

Majadiliano kati ya rais wa Syria na mkuu wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu Septemba 10.2011.
Majadiliano kati ya rais wa Syria na mkuu wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu Septemba 10.2011. REUTERS/Sana/Handout

Umoja wa nchi za Kiarabu pamoja na Uturuki zimeendelea kuongeza shinikizo zaidi kwa serikali ya Syria wakitaka kusitishwa kwa mauaji ya raia yanayofanywa na vikosi vya serikali katika miji mbalimbali nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Akihutubia mkutano wa baraza la Umoja huo mjini Cairo Misri, waziri mkuu wa Uturuki, Raccep Tayyep Erdogan amesema kuwa wakati umefika sasa kwa rais Bashar al-Asad kukubali mabadiliko ama yeye mwenyewe kuondoka mamlakani.

Viongozi hao wameonya nchi hiyo kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe hali itakayochangia kushindwa kupatikana kwa suluhu ya kudumu katika nchi hiyo.