Togo-Mahakama

Mahakama nchini Togo yatoa hukumu kwa washukiwa wa jaribio la mapinduzi

Kpatcha Gnassingbé, ndugu wa wa rais wa Togo wakati alipokuwa waziri wa ulinzi
Kpatcha Gnassingbé, ndugu wa wa rais wa Togo wakati alipokuwa waziri wa ulinzi (Photo : AFP)

Mahakama kuu nchini Togo hatimaye imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 20 kila mmoja dhidi ya viongozi wa zamani wa taifa hilo waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na kupanga njama za kutaka kuipindua serikali ya rais Faure Gnassibe mwaka 2009.

Matangazo ya kibiashara

Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Petchelebia Abalo ametoa hukumu hiyo kwa aliyekuwa waziri wa ulinzi Kpatcha Gnassingbé ambaye ni kaka wa rais Faure Gnassingbé, Jenerali Assani Tidjani na Abi Atti ambao wote kwa kila mmoja atatumikia kifungo hicho.

Mahakama hiyo pia imewafutia mashtaka watuhumiwa wengine 20 baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kuwahusisha moja kwa moja na tukio hilo huku watuhumiwa wengine wakipewa hukumu ya vifungo tofauti kwa kuhusika kwao kwenye mpango huo.