Libya

Waasi wa Libya wafaanikiwa kusonga mbele na kuuteka mji wa Sabha

Wapiganaji wa vikosi vya waasi nchini Libya
Wapiganaji wa vikosi vya waasi nchini Libya Reuters

Vikosi vya waasi nchini Libya vimeelezwa kusonga mbele na sasa vinaushikilia mji wa Sabha ulioko kusini mwa mji wa Bani Walidi. Mapambano makali yaripotiwa huku waasi hao wa Libya waki kiri kupata upinzani mkali katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la waasi kanali Ahmed Bani amesema kuwa vikosi vyake vimefanikiwa kusonga mbele licha ya upinzani mkali na kuongeza kuwa wanashindwa kufanya mashambulizi ya nguvu katika mji wa Sirte kutokana na raia wengi kukwama katika mji huo.

Wakati huohuo waasi wamesema kuwa wameanza operesheni ya kuuteka mji wa Oasisi unaoamika kuwa mtoto wa kanali Muamar Gaddafi Seif al-Islam Gaddafi ndiko amejificha.

Hata hivyo waasi hao wamekiri vita hivyo kuwa vingumu katika miji hiyo miwili ukilinganisha na miji mingine ambapo wamesema kwenye miji hiyo kuna ngome kubwa ya wafuasi wa kanali Gaddafi.