Zambia

Upinzani waongoza katika matokeo ya muda ya uchaguzi nchini Zambia

RFI, NDEKETELA

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini zambia ametoa matokeo ya awali ya kura za urais zilizopigwa zikionesha Mpinzani wa Rupia Banda, Michael Sata akiongoza.Na Muandishi wetu nchini Zambia Edwin David Ndeketela

Matangazo ya kibiashara

Irene Mambilima amewaambia waandishi wa habari kuwa matokeo hayo ni ya maeneo 33 kati ya 150 na michael Sata anaongoza kwa kura laki 2 sitini na 5 elfu mia nane na 43 dhidi ya laki moja 92 elfu mia 966 za Banda

Hakuna vyama vingine vya upinzani vilivyojitwalia zaidi ya kura laki moja.

Mambilima amesema Matokeo zaidi yataendelea kutolewa hii leo.