Sudani

Wanajeshi wa Sudani wapambana na waasi katika mji wa Blue Nile

Msemaji wa jeshi la Sudani
Msemaji wa jeshi la Sudani RFI

Jeshi la Sudani hapo jana lilikuwa kwenye mapigano makali na waasi katika mpaka ulio na mgogoro wa Blue Nile, msemaji wa jeshi hilo Sawarmi Khaled amethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Khaled amesema kuwa hivi sasa majeshi yanadhibiti eneo la Dindiro na kukamata vifaru vitano na magari manne ya waasi.

Msemaji huyo amesema waasi waliweka vikosi vyao vingi ili kuzuia majeshi ya Sudan kuingia eneo la Kurmuk, katika mpaka kati ya Sudan na Ethiopia.

Kama ilivyo kwa kodofan kusini, Blue Nile imekuwa ikigombewa katika mgogoro wa miaka 22 kati ya Khartoum na waasi wa kusini.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema mapigano katika eneo la Blue Nile, yamesababisha takriban raia elfu 50 kuyakimbia makazi yao.