Senegal

Chama tawala nchini Sengal, chasitisha maandamano ya kisiasa

Maandamano ya upinzani jijini Dakar kwa ajili amani Casamance Agosti 2010.
Maandamano ya upinzani jijini Dakar kwa ajili amani Casamance Agosti 2010. SEYLLOU / AFP

Chama tawala cha nchini Senegal kimesema kinasitisha maandamano yote ya kisiasa nchini humo, tangazo lililokuja siku moja kabla ya upinzani nchini humo kupanga kufanya maandamano kudai mabadiliko ya, utawala nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe uliotumwa kwa wanahabari kwa njia ya nukushi, chama tawala cha Senegalese Democratic Party kimesema maandamano ya kisiasa yamesitishwa baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi ndani ya bunge la nchi hiyo Diawar Toure.

Kutokana na kuwepo kwa maombolezo ya kifo chake, mkurugenzi wa kamati ya chama cha PDS amesema wanaahirisha shughuli za chama mpaka itakapotolewa taarifa tena.

Maandamano leo hii yalipangwa kuwa sambamba na mengine makubwa yaliyoandaliwa na makundi ya upinzani, msemaji wa chama cha upinzani Mustafa Niasse amesema kundi la upinzani litaendelea na maandamano hii leo

upinzani nchini humo hufanya maandamano kila ifikapo tarehe 23 ya kila mwezi kumtaka rais wa taifa hilo Abdoulaye Wade kuachia madaraka.