Morocco-Marakech

Mshukiwa mku wa shambulio la Marakech apinga kuhusika kwake

mshukiwa mkuu wa kesi ya shambulio la Bomu lililogharimu maisha ya watu 17 mjini marakkesh nchini Morocco amepinga kuhusika na shambulio hilo na kuiambia mahakama kuwa hizo ni njama za vyombo vya kiintelijensia.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lililotekelezwa mwezi April mjini humo liligarimu maisha ya watu waliokuwa katika mgahawa wengi wao watalii wa kigeni.

Adel Othmani atakayekabiliwa na hukumu ya kifo iwapo atabainika kuhusika na shambulio hilo,amekana kutekeleza mauaji, na kutengeneza milipuko, huku wengine saba walioshtakiwa sambamba nae wakikana kushiriki katika shambulio hilo.

Kesi hiyo imeahirishwa.

Mlipuko wa bomu ulitokea katika mgahawa wa Djemaa El-Fna, mjini Marrakesh na kuua raia wanane waufaransa,wawili wa morocco, na raia wengine wa uingereza ,Canada,Switzerland,ureno na uholanzi.