Nigeria

Serikali ya Nigeria yatakiwa kufikia makubaliano na kundi la Boko Haramu

RFI

Tume maalumu ya kusimamia mazungumzo kati ya serikali ya Nigeria na kundi la kiislamu lenye msimamo mkali nchini humo la Boko Haramu iliyoundwa siku ya jumatatu, imesisitiza serikali kukubali kufikia muafaka na kundi hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kamati hiyo ambayo iliundwa na rais Goodluck Jonathan miezi miwili iliyopita ilikuwa ikiwasilisha ripoti yake kwa makamu wa rais Namadi Sambo ambaye nae ameahidi serikali yake kufanyia kazi mapendekezo ya tume hiyo.

Akiongea mara baada ya kukabidhi ripoti ya tume yake mwenyekiti wa kamati hiyo Usman Galtimari amesema kuwa njia pekee ambayo serikali inaweza fikia kumaliza hali tete ya kiusalama kati yake na boko haramu ni kwa kufanya mazungumzo na viongozi wa kundi hilo na kusikiliza madai yao.