Pata taarifa kuu
Cote d'Ivoire

Rais wa Côte d’Ivoire kuzindua shughuli za tume ya Majadiliano, Ukweli na Maridhiano

RFI
Ujumbe kutoka: Ali Bilali
Dakika 2

Wananchi wa Côte d’Ivoire wanatarajiwa kushuhudia Rais Alassane Ouattara akizundua rasmi shughuli za Tume ya Majadiliano Ukweli na Maridhiano inayoongozwa na Charles Konan Banny ambayo itakuwa na kibarua cha kuwapatanisha wananchi baada ya kushuhudia machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka jana. Wajumbe 11 wanaounda tume hiyo tayari wanatambulika, akiwemo mchezaji wa soka la kimataifa Didier Drogba

Matangazo ya kibiashara

Tayari wajumbe wa Tume hiyo wametakiwa kuhakikisha wanatekeleza kwa umakini majukumu ambayo wamekabidhiwa na sasa Askofu wa Afrika Kusini Desmond Tutu ni miongoni mwa waliotoa kauli hiyo.

Askofu Tutu amesema kuwa Tume hiyo ya  Ukweli na Maridhiano inatakiwa imalize hali ya kutokuelewana iliyozuka kutoka kwa wafuasi wa Laurent Gbgabo na wale wa Rais wa sasa Ouattara.

Hata hivyo kumekuwa na maoni tofauti kuhusu majukumu ya tume hiyo ambayo haijaanza shughuli zake na ambazo huenda zikachukuw amuda ili zianze, lakini hata hivyo mahakama nchini humo imeanza kazi zake.

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagba na wafuasi wake wanazuiliwa kwa makosa ya kuhujumu mali ya umaa na kuyumbisha usalama wa taifa, ambapo sasa wachambuzi wa mambo wanahoji nafasi ya tume hiyo kwenye vyombo vya sheria.

Kumekuwa utatanishi kuhusu mshtumiwa anaweza kusamehewa kupitia tume hiyo wakati ambapo amehukumiwa na mahakama ya nchini humo au ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC. Hata hivyo nchini humo kila pande iko tayari kwa maridhiano.

Maoni kutoka upande wa ikulu ya nchi hiyo ni kwamba msamaha kupitia tume hiyo ufikiwe baada ya mtuhumiwa kuhukumiwa au kukatiwa kesi na vyombo vya sheria, jambo ambalo upande wa rais wa zamani wanasema tume hiyo kufikia ufanisi ni kuacha kwanza huru Laurent Gbagbo na watu wake wa karibu.

Ilikuonyesha kupuuzia juhudi hizo, rais wa zamani Laurent Gbagbo ameomba Umoja wa Mataifa kuunda tume itayo chunguza maovu yote yaliontendeka nchini Côte d’Ivoire tangu mwaka 2002.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.