Swaziland

Mfalme Mswati wa 3 amsimamisha kazi jaji mkuu wa nchi hiyo

Mfalme wa Swazland Mswati III
Mfalme wa Swazland Mswati III

Mfalme Mswati wa 3 wa Swaziland imemsimamisha kazi jaji anayeelezwa kuwa mkosoaji mkubwa wa idara ya mahakama ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Jaji thomas Masuku aliwahi kusimamishwa kazi kwa muda mwezi june,na sasa anakabiliwa na shutma kadhaa ikiwemo kumdhihaki mfalme mswati,mwaka jana.

Katibu wa Tume ya mahakama JSC ,Lorraine Hlophe amesema tume hiyo ilipendekeza Masuku asimamishwe kazi kwa muda wa miezi mitatu, mfalme Mswati akaidhinisha uamuzi huo wa tume.

Masuku ni mmoja wa majaji wachache wenye kuthubutu kukosoa utawala wa mswati, huku ikielezwa kuwa wanasheria wa Swaziland wamegoma kupinga kusimamishwa kazi kwa jaji huyo,na kushinikiza kuondolewa kwa jaji mkuu wa nchi hiyo kwa namna anavyolishughulikia swala hilo.