Zambia

Rais mpya wa Zambia atangaza baraza lake la mawaziri

Tunisienews

Rais mpya wa Zambia Michael Sata hatimaye ametangaza Baraza lake la Mawaziri likiwa na mawaziri kumi na kenda akimjumuisha mfanyabiashara na mchumi mahiri Alexander Chikwanda anayekuwa Waziri wa Fedha.

Matangazo ya kibiashara

Rais Sata amechagua Baraza lake la Mawaziri ambalo limejaa mabadiliko mengi kama ambavyo ilikuwa inatarajiwa huku nafasi ya Makamu wa Rais akimchangua Guy Scott ambaye msaidizi wake kutoka Chama Cha PF.

Baraza la Mawaziri linatarajiwa kuapisha hiyo kesho huku Manaibu Waziri wengi waliokuwa wanahudumu kwenye serikali iliyopita wamekabidhiwa jukumu la kuondoka wizara hizo na kuleta mabadiliko kwa wananchi.