Côte d’Ivoire

Spika wa bunge la Côte d’Ivoire amtaka rais wa nchi hiyo kukutana na rais wa zamani Laurent Gbagbo

Mamadou Koulibaly,Spika wa bunge la Côte d’Ivoire
Mamadou Koulibaly,Spika wa bunge la Côte d’Ivoire AFP PHOTO ISSOUF SANOGO

Spika wa Bunge la Cote D'Ivoire Mamadou Koulibaly amewataka Rais wa sasa Alassane Ouattara na wapinzani wake Laurent Gbagbo na Henri Konan Bedie kukutana kwa ajili ya mazungumzo ya maridhiano.

Matangazo ya kibiashara

Spika Koulibaly amesema kile ambacho kinaendelea nchini Cote D'Ivoire ni mgogoro wa kisiasa na si suala la kikabila kama ambalo limekuwa likisema na kuchangia chuki baina viongozi hao watatu.

Kiongozi huyo wa Bunge amesema kile ambacho kinaonekana baina ya viongozi hao watatu ni kutawaliwa na masuala ya kikabila, kidini na hata kikanda ambayo yanachochea hali ya utulivu kukosekana.

Hapo jana rais wa nchi hiyo alizindua rasmi shughuli za tume ya majadiliano ukweli na maridhiano yenye kuundwa na wajumbe 11 ikiongozwa na waziri mkuu wa zamani Charles Konan Banny