Libya

Makamu wa Rais wa Sudan atua Libya, NTC wajigamba kuteka uwanja wa ndege

Reuters

Makamu wa rais wa Sudan, Ali Osman Taha yuko Tripoli kukutana na viongozi wa serikali ya mpito nchini humo.Taha anakuwa kiongozi wa juu wa Sudan,kuzuru Libya tangu juhudi za mapinduzi zilipoanza mapema mwaka huu,katika ziara inayolezwa ni ya kusiistiza uhusiano kati ya mataifa haya mawili.

Matangazo ya kibiashara

 

Mwezi Agosti mwaka huu waziir wa nchi za kigeni wa Sudan,alikutana na kiongozi wa baraza la serikali ya mpito nchhini Libya,Mustafa Abdel Jalil, aliyenukuliwa kuwa,serikali ya Khartoum ilitoa msaasda wa kijeshi kwa waasi.

Wakati huohuo wapiganaji wa Serikali ya Mpito nchini Libya NTC ambayo inapambana kuweka kwenye himaya yake Miji iliyosalia chini ya askari watiifu kwa Kanali Muammar Gaddafi wametangaza kuchukua umiliki wa Uwanja wa Ndege katika Jiji la Sirte.

Wapiganaji hao wamesema baada ya mapambano makali wamefanikiwa kuurejesha tena Uwanja huo wa ndege kwenye himaya yao baada ya hao awali askari watiifu wa Kanali Gaddafi kufanikiwa kuupora.

Mapambano haya yanaendelea kuchacha wakati huu ambapo Maseneta wa Marekani kutoka Chama Cha Republican wakiwa wamezuru nchini Libya na kukutana na viongozi wa NTC huku Seneta John McCain akipongeza mapinduzi hayo.