Libya

Raia wazidi kukimbia mji Sirte wakati NTC wakiendeleza mashambulizi

Reuters/Esam Al-Fetori

Mgogoro wa Libya bado umeendelea kuleta wasiwasi kwa wananchi wake wakati majeshi ya Baraza la Mpito la Libya, NTC yakiendeleza mapambano ya kuuweka katika himaya yao mji wa Sirte.

Matangazo ya kibiashara

 

 

Raia wa Libya wamelazimika kuukimbia mji wa Sirte alimozaliwa kanali Muammar Gaddafi hapo jana kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya serikali mpya ya NTC na wapiganaji wa Gaddafi.

Magari yaliyokuwa yamebeba familia zilizoacha makazi yao mjini Sirte yameonekana katika mistari mirefu ikipita katika maeneo ya ukaguzi katika njia ya kuelekea nje ya mji huo wakikaguliwa mizigo waliyobeba na vitambulisho vyao.

Mjini Cairo nchini Misri Waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panneta amesema operesheni ya majeshi ya kujihami ya nchi za magharibi, NATO lazima iendelee nchini Libya kwa kuwa bado mapigano ya ardhini yanaendelea.