Kenya-Somalia

Serikali ya Kenya na harakati za kuwatafuta watalii walIotekwa nyara

Reuters/Thomas Mukoya

Serikali ya Kenya imeweka bayana ipo katika hatua nzuri kuweza kuwapata watalii wawili ambao wametekwa nyara katika Pwani ya Mji wa Lamu wakati huu ambazo zoezi la kuwasaka likiendelea kupamba moto.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Kenya Mwai Emilio Kibaki amelazimika kuitisha kikao cha dharura na wadau wa vyombo vya usalama kwa ajili ya kusaka suluhu ya namna ya kuwapata watu hao ambao wameteka huko Lamu.

Jeshi la Polisi kupitia kwa Msemaji wake Charles Owino limethibtisha kuwa katika mkakati mzuri wa kuweza kuwapata watu hao ambao wametekwa nyara kwa zaidi ya juma moja sasa.