Mustafa Abdeljalil afanya mazungumzo na askari wa kanali Gaddafi.
Imechapishwa:
Kiongozi wa baraza la mpito la NTC nchini Libya Mustafa Abdeljalil a jana katika mji wa Sirte kuonana na wapiganaji wanaopambana na askari tiifu kwa kanali Muamar Gaddafi. Mazungumzo na wapiganaji hao yalidumu muda wa saa mbili.
Wapiganaji hao wa baraza la mpito wanajigamba kuyateka maeneo muhimu ya jiji hilo la sirte baada ya kuwasambaratisha wapiganaji wa Gaddafi. Hapo jana mapambano yalidumu muda wa saa mbili. Hata hivyo mji huio wa Sirte aliko zaliwa kanali Gaddafi haujakombolewa wote.
Hayo yakijri, wawakilishi wa viwanda vya ujenzi vya nchini Ufaransa wapatao thamanini, wamejielekeza jiji Tripoli kukutana na viongozi wa baraza la mpito kuangalia uweszekano wa ukarabati wa nchi hiyo.