MALAWI-SUDANI

Umoja wa mataifa waitaka Malawi kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir

Mkuu wa sera za kigeni wa baraza la umoja wa ulaya,Catherine Ashton.
Mkuu wa sera za kigeni wa baraza la umoja wa ulaya,Catherine Ashton. REUTERS/Vincent Kessler

Mkuu wa Umoja wa Ulaya anaehusika na sera za kigeni Catherine Ashton ameitaka serikali ya Malawi imkamate Rais wa Sudan Omar al-Bashir ambaye anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita wakati akiwa ziarani nchini humo kwa sasa.

Matangazo ya kibiashara

Ashton amesema kuwa Malawi ni mwanachama wa Mkataba wa Roma ambao uliagiza kuanzishwa kwa mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, hivyo Malawi inatakiwa kuheshimu majukumu yake chini ya sheria za kimataifa kwa kumkamata Bashir.

Bashir aliwasili nchini Malawi jana Alhamisi kwa ajili ya kushiriki mkutano wa kilele wa biashara ya kikanda, ambapo alipokelewa na kukaribishwa na ulinzi mkali wa kijeshi.

Bashir ni rais wa kwanza aliyepo madarakani kushitakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ambayo ilitoa kibali cha kukamatwa kwake kwa tuhuma za mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita uliotekelezwa katika jimbo la Darfour.