Chama cha ANC nchini Afrika kusini chawasilisha rufaa ya kutaka kuimbwa wimbo uliopigwa marufuku
Chama tawala nchini Afrika kusini cha Afrikan National Congress kimetangaza kuwasilisha rufaa yake katika mahakama kuu ya katiba nchini humo kutaka kuruhusiwa kuimba wimbo ambao ulipigwa marufuku mwezi mmoja uliopita.
Imechapishwa:
Msemaji wa chama hicho, Keith Khoza amesema kuwa watawasilisha rufaa yao juma hili katika mahakama ya katiba kupinga wimbo wao waliouita wa uhuru kupigwa marufuku na mahakama kuu kwa kile ilichodaiwa kuwa na maneno ya kichochezi na kibaguzi dhidi ya watu weupe.
Lakini licha ya wimbo huo kupigwa marufuku na mahakama kuu vijana nchini humo wamekuwa wakiuimba mara kwa mara kwenye maeneo ya wazi katika kile kinachoonekana kupinga huku hiyo.