Benin-Nigeria

Rais wa Benin ziarani nchini Nigeria

Rais wa Benin Thomas Boni Yayi yupo nchini Nigeria kwa ziara ya kikazi ambapo amekutana na rais Goodluck Jonathan na kufanya nae mazungumzo kuhusu hali ya uharamia katika ukanda wa nchi za afrika magharibi.

Ma rais wa Benin Boni Yayi na wa Nigeria Goodluck Jonathan
Ma rais wa Benin Boni Yayi na wa Nigeria Goodluck Jonathan journaldutchad
Matangazo ya kibiashara

Akiongea na waandishi wa habari mjini Abuja rais Yayi amesema kuwa lengo kubwa la ziara yake ni kujadili ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa yao lakini suala la uharamia walilipa kipaumbele katika mazungumzo yao kutokana na hivi karibuni kuongezeka kwa matukio ya uharamia katika pwani za bahari zao.

Tarehe 8 ya mwezi huu maharamia wanaosadikiwa kutoka katika pwani ya bahari ya somalia waliiteka meli moja ya mafuta pamoja na wafanyakazi wake zaidi ya ishirini kabla ya kutangaza kuiachia ijumaa ya wiki iliyopita bila ya taarifa zozote za sababu ya kufanya hivyo.

Nchi za Afrika magharibi zimeanzisha sheria ya pamoja ya kupambana na maharamia katika owani ya bahari zao kwa lengo la kukabiliana na uharamia.