Wanajeshi watano wa Kenya wauawa kwa ajali ya Helicopta, wakati wa harakatiza kuwasaka wapiganaji wa Al Shabab
Serikali ya Kenya imethibitisha kwamba wanajeshi wake wameingia nchi jirani ya Somalia kuwasaka wanamgambo wa Al ShabaAb. Katibu Mkuu wa wizara ya usalama nchini Kenya , Francis Kimemia, amesema kuwa wanajeshi wao waliingia nchini Somalia siku ya Jumapili, kuwasaka wapiganaji wa Al Shabaab, ambao wanatuhumiwa kuwateka nyara raia wanne wa kigeni ndani ya Kenya.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Katibu huyo mkuu wa wizara ya usalama nchini Kenya amesema Tayari Al Shabab wameshambulia Kenya. Wameingia ndani ya nchi, wakapiga risasi na kuchukua marafiki wa Kenya. Ameongeza kuwa Kenya iko tayari kuwasaka wanamgambo hao popote walikojificha ndani ya Somalia.
Hii ni mara ya kwanza rasmi Vikosi vya Kenya vinaingilia kijeshi nchini Somalia tangu mwanzo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1991.
Katika mkoa wa kusini wa Juba, majeshi ya Kenya, yameonekana kuungwa mkono na askari wa serikali ya mpito ya Somalia pamoja na wanamgambo wa ndani, walionekana karibu na mji wa Qoqani. Mji ambao ni ngome ya wapiganaji wa Al Shabab kwenye kilometa kadhaa mpakani mwa Kenya na Somallia.
Mashahindi wanasema wameona asakri wa Kenya wakiingia nchini Somalia na magari ya kijeshi yakibeba mizinga na makombora. Huku wengine wakithibitisha kuwaona askari wa kenya wakichimba mitaro karibu na mji wa Qoqani
Jumapili, msemaji wa serikali ya Kenya, Alfred Matua, alitangaza kuingia kwa jeshi la Kenya nchini Somalia, kuwasaka wapiganaji wa Al Shabab ambayo inahusika na vitendo vya utekaji nyara na mashambuzli kadhaa katika ardhi ya Kenya.
Mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo inaharibu utekelezwaji wa operesheni hiyo.
Wakati hayo yakiarifiwa Jeshi la Kenya limewapoteza wanajeshi wake watano katika ajali ya ndege iliotokea usiku wa Jumapili karibu na mji wa Kenya wa Liboi, umbali wa kilomita ishirini kutoka mpakani.
Meja Emmanuel Chirche amesema kwamba Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kulikuwa na tatizo la kiufundi.