Swaziland

Mfalme Mswati afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri

/AFP PABALLO THEKISO

Mfalme Mswati wa Swaziland ametangaza kufanya mabadiliko makubwa katika serikali yake kwa kuwafuta kazi baadhi ya mawaziri na kuwatangaza mawaziri wapya watakaounda serikali.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa serikali imesema kuwa mfalme Mswati amewafuta kazi mawaziri kadhaa akiwemo waziri wake sheria David Matse ambaye hivi karibuni alikataa kumfukuza kazi jaji mmoja katika mahakama kuu pamoja na waziri wa habari Nelisiwe Shongwe ambaye nae amekumbana na kadhia hiyo ya mfalme.

Akinukuliwa na vyombo vya habari waziri mkuu wa nchi hiyo Barnabas Dlamini amesema kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuwa na viongozi ambao wanasikiliza wanachoagizwa na mfalme pamoja na kuondoa viongozi wasio watendaji katika wizara zao.

Wachambuzi wa mambo tayari wamekosoa hatua hiyo ya Mfalme Mswati wakisema ni udhalilishaji huku licha ya kubadili mawaziri hao bado serikali yake imeendelea kukosolewa kwa kushindwa kuimarisha uchumi wa taifa hilo.