Afrika ya kati

Amnesty International yatowa ripoti inayoishutumu serikali ya Afrika ya kati kushindwa kuwalinda raia wake

Shirika la kimataifa linalosimamia haki za binadamu duniani la Amnesty International limetoa ripoti inayokosoa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya kati kwa kushindwa kuwalinda raia wake na kuzua vurugu za mara kwa mara nchini humo.

Im
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa shirika hilo katika kitengo cha utafiti kwa Afrika ya kati Godfrey Byaruhanga amesema kuwa utafiti uliofanywa na shirika lake hivi karibu nchini humo umebaini kuwepo ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na vikosi vya usalama.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa kuna zaidi ya vikundi vya waasi 14 nchini humo lakini serikali imeshindwa kuonyesha juhudi zozote za kukabilina navyo na badala yake baadhi yao vimekuwa vikifanya mauaji ya raia wasio na hatia.

Ni hapo jana tu vikundi viwili vya waasi vilitiliana saini ya kusitisha mapigano katika eneo la mji wa Bria eneo ambalo kundi la Lords Resistance Army ambalo asili yake ni nchini Uganda linaelezwa kuendesha mapigano katika nchi hiyo.