Mali

Baraza la mawaziri nchini Mali laafiki kuhusu tarehe rasmi ya uchaguzi nchini humo

Baraza la mawaziri nchini Mali hatimaye limekubaliana na kupitisha tarehe 29 ya mwezi wa 4 hapo mwakani nchi hiyo kufanya uchaguzi wake wa duru la kwanza la Urais pamoja na kuanza mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya.

Matangazo ya kibiashara

Tayari joto la kinyang'anyiro limeanza kupanda kwa vyama mbalimbali kuwatangaza wagombea wao huku chama cha Alliance for Democracy ADEMA kikimtangaza spika wa bunge Dioncounda Traore kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwakani.

Amadou Toumani Toure ambaye ni rais wa sasa wa mali aliteuliwa kidemokrasia kwa mara ya kwanza mwaka 2002 ambapo anatarajiwa kuachia nafasi hiyo huku uchaguzi wa wabunge ukipangwa kufanyika mwezi wa saba mwakani.