Mahakama kuu nchini Cameroon yatupilia mbali ombi la upinzani la kuzuia kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi
Mahakama kuu nchini Cameroon imetupilia mbali maombi ya kambi ya upinzani nchini humo waliotaka mahakama hiyo kuzuia utangazwaji na uchapishwaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika juma moja lililopita, huku wengine wakiomba uchaguzi huo ufutwe na uandaliwe mwingine.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Malalamiko hayo yaliwasilishwa mahakamani na chama cha upinzani cha Social Democratic Front SDF kinachoongozwa na John Fru Ndi ambapo aliwasilisha malalamiko kumi na 8 huku mengine yakiondolewa na vyama vya upinzani vilivyokuwa vikipinga kutangazwa kwa matokeo hayo.
Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa hapo kesho huku chama tawala cha rais Paul Biya kikitarajiwa kutangazwa mshindi.
Rais Biya amekaa madarakani kwa miaka 29 mpaka sasa.