Kenya

Serikali ya Kenya na maadhimisho ya siku ya mashujaa

Wakenya wameadhimisha sikuuu ya Mashujaa hivi leo kuwakumbuka wale wote waliopigania uhuru wa taifa hilo, na siku hii imeadhimihswa kwa mara ya pili tangu taifa hilo lilipopata katiba mpya mwaka jana. Sherehe zimefanyika katika uwanja wa nyayo chini ya ulinzi mkali wa usalama kukihofiwa mashambulizi ya wanamgambo wa al Shabab. 

Billy
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Uslama lililazimika kumsaka kila raia alikwenda kuhudhuria sherehe hizo za maadhimisho ya siku ya mashujaa. Milango ya uwanja huo ilifungwa mapema wakati kundu kubwa la watu walikuwa nje ya uwanja huo wakihitaji kuhudhuria sherehe hizo.

Licha ya mvua ilionyesha, wananchi waliojitokeza walivulia katika maeneo walipokuwa wamekaa ambapo hakuna alieingia na kuruhusiwa kuondoka kabla ya sherehe kufikia tamati.

Viongozi wa serikali ya Kenya walihudhuria sherehe hizo na kutumia fursa ya kusema kuwa Serikali ya Kenya itatumia kila kitu kilicho ndani ya uwezo wake kukabiliana na wanagambao wa Al-Shabab kutoka Somalia.

Rais Mwai Kibaki amesema majeshi ya Kenya ambayo kwa sasa yako Somalia kusaka wanagambo hao yataendeleza operesheni hiyo kwa lengo la kutokomeza wanamgambo hao wa Al Shabab.

Matamshi hayo ya rais Kibaki pia yaliungwa mkono na waziri Mkuu wa nchi hiyo Raila Odinga.

kuhusu kifo cha raia wa Ufaransa Marie Dedieu mikononi mwa wanagambo wa AL-Shabab wanaoaminiwa kumteka nyara wiki mbili zilizopita, rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameshutumu watekaji nyara hao wanaotaka kikombozi au malipo kabla ya kutoa mwili wa raia huyo aliyetekwa nyara katika kisiwa cha lamu pwani ya Kenya.