Viongozi wa Libya watangaza kuikomboa nchi na sasa wajipanga katika vita vya kisiasa
Imechapishwa: Imehaririwa:
Utawala mpya nchini Libya kupitia Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Taifa NTC limetoa onyo la uwepo wa vita ya kisiasa katika nchi hiyo lakini wao wamejipanga vyema kuweza kukabiliana na hali hiyo.
Mahmud Jibril Makamu Mwenyekiti wa NTC ndiye ambaye ametoa onyo hilo na kuweka bayana wao wamejipanga vyema kuhakikisha vita hiyo ya kisiasa inashindwa na watakuja na sheria mpya.
Jibril ameweka bayana wamemaliza vita ya kuiweka huru Libya na sasa wamehamia kwenye vita vya kisiasa ambavyo zitakuwepo wakati huu ambapo taifa hilo halijajengwa upya lakini wakishafanya hivyo wayakuwa wamefanikiwa.
Kiongozi huyo amesema hali jiyo isipochukuliwa kwa umakini wake basi ni wazi kabisa machafuko yanaweza kuendelea kuchukua nafasi katika nchi hiyo iliyokuwa chini ya Kanali Muammar Gaddafi kwa miaka arobaini na miwili.
Kauli hiyo inakuja wakati bado wapiganaji wa NTC wanaendelea kupambana na askari watiifu wa Kanali Gaddafi katika ngome zao imara zilizopo katika Miji wa Sirte na Bani Walid.