Kampeni za uchaguzi wa bunge na rais za zinduliwa kwa vurugu katika mji wa Mbuji May
Mtu mmoja ameuawa wengine watatu wamejeruhiwa kwa risase jana octoba 28 katika mji wa Mbuji May wakati wa kampeni za uchaguzi wa chama cha wafanyakazi kwenye uchaguzi wa rais na wa bunge wa Novemba 28 mwaka huu.
Imechapishwa:
Kwa mujibu wa mashahidi waliozungumza na RFI, Wafuasi wa upinzani walimiminika barabarani kusherehekea kuanzishwa kwa kampeni za uchaguzi. Polisi katika eneo hilo ilijaribu kuwasambaratisha bila mafaaniko, na ndipo kuwafyatulia risase.
Baada ya tukio hilo, wananchi wenye hasira walivamia makaaazi ya wajumbe wa chama madarakani jijini Mbuji may makao makuu ya Kasai Mashariki ngome ya mpinzani mkuu wa serikali Etienne Tshisekedi wa Mulumba wa chama cha UDPS.
Akionekana kuguswa zaidi na tukio hilo Roger Meece mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC ameitaka serikali ya Kinshasa kuanzisha uchunguzi haraka kabla ya kukumbusha kwamba uhuru wa kukusanyika, kujadiliana kisiasa na uhuru wa kujitetea lazima vilindwe katika kipindi hiki cha kampeni