KENYA

Majeshi ya Kenya yatuhumiwa kuua raia nchini Somalia

Watu watano wanashukiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 45 wamejeruhiwa vibaya kufuatia shambulio la anga lililofanywa na ndege za Kenya katika kambi moja mpakani wa Somalia nchi hiyo.,

Mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Julius Karangi
Mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Julius Karangi Online
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika moja la kibinaadamu nchini Kenya la MSF imesema kuwa wanaushahidi wa kutosha unaodhibitisha kuwa ndege za jeshi la Kenya zilishambulia kambi ya Jibil ambayo inahifadhi wanawake na watoto.

Taarifa za shirika hilo la kibinaadamu pia zilizdhibitishwa na wakuu wa jeshi la Kenya ambao walikiri kufanya shambulio katika eneo la Jibil ingawa hawakuweka wazi endapo shambulio hilo liliua raia wa kawaida au wafuasi wa kundi la Al-Shabab.

Hata hivyo waziri mkuu wa Somalia Abdiwelli Mohammed Ali ambaye yuko nchini Kenya kwa mazungumzo amesema kuwa haamini kama majeshi ya Kenya yanaweza kushambulia raia wa kawaida na kwamba analifuatilia sula hilo kwa ukaribu.

Waziri mkuu Mohammed Ali amewasili nchini Kenya hii leo akiongozana na viongozi kadhaa wa serikali ambapo watakutana na viongozi wa Kenya kuzungumzia operesheni ambayo inafanywa na majeshi hayo nchini Somalia.

Awali kulikuwa na mvutano mkali wa maneno baada ya rais wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed kusema wazi kuwa haungi mkono operesheni ambazo zinafanywa na majeshi ya hayo nchini mwake.

Kwa upande wake mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Julius Karangi amesema kuwa hakuna muda maalumu ambao jeshi lake limepanga kuviondoa vikosi vyake nchini Somalia badala yake vitaendelea kusalia mpaka pale utakapokuwepo uhakika kuwa wapiganaji wa Al-Shabab wametokomezwa nchini Somalia.