Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe aionya Swazirland kutokana na hatuwa yake ya kumyima visa mkewe

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, jijini Harare, Februari 17, 2010
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, jijini Harare, Februari 17, 2010 Reuters/Philimon Bulawayo

Rais wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe ametoa onyo kwa serikali ya Switzerland huenda ikapoteza mali zake ambazo zipo katika nchi yake kutokana na taifa hilo kukataa kutoa visa kwa mkewe na viongozi wengine wa juu ambao walikuwa wanatakiwa kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa UN.

Matangazo ya kibiashara

Rais Mugabe amesema kwa sasa nchi ya Switzerland imeanza kuonesha ina uovu na kwa hiyo iwapo wataendelea na mwenendo huo ni wazi watataifisha mali zote ambazo zipo katika taifa hilo zinazomilikiwa na nchi hiyo.

Kauli ya Rais Mugabe imekuja baada ya mkewe Grace, mlinzi wake pamoja na viongozi wengine wanne ambao alipaswa kuhudhuria nao mkutano wa UN kukataliwa visa ya kuingia nchini Switzerland.