Sudan-Kordofan

Waasi wa SPLM wauawa katika mapambano na wanajeshi wa Sudani

Waasi wakiimba kwa kishindo « Al Bashir utasikia sauti ya wananchi wa Nuba ».
Waasi wakiimba kwa kishindo « Al Bashir utasikia sauti ya wananchi wa Nuba ». RFI/Stéphanie Braquehais

Mamia ya Waasi wa Kundi la SPLM lenye maskani yake Kaskazini mwa Sudan wamepoteza maisha kwenye mapambanao ambayo yamezuka kati yao na wanajeshi wa Sudan katika eneo la Kordofan Kusini lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Matangazo ya kibiashara

Gavana wa Jimbo la Kordofan Kusini Ahmed Haroun na Msemaji wa Jeshi la Nchi hiyo Sawarmi Khaled Saad wamethibitisha vifo hivyo vya wapiganaji wa Kundi la Waasi la SPLM mia saba waliouawa kwenye mashambulizi hayo yaliyotokea katika Jiji la Teludi.

Thabo Mbeki ni Rais wa zamani wa Afrika Kusini lakini kwa sasa anajukumu la kupatanisha Sudan Kaskazini na Kusini na hapa anaeleza kile ambacho kinaendelea.