KENYA

Majeshi ya Kenya yajiandaa na mashambulizi zaidi dhidi ya Al-Shabab nchini Somalia

Reuters/Noor Khamis

Jeshi la Kenya kupitia Msemaji wake Emmanuel Chirchir limetoa onyo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ya kwamba inajiandaa kufanya mashambulizi ya kijeshi mfululizo kwenye miji kumi nchini Somalia.

Matangazo ya kibiashara

Meja Chirchir amesema hayo katika ukurasa wake wa twitter kuwa maeneo hayo hali kadhalika mjini Badheere, Barawe, Jilib na Afmadow yatakumbwa ma mashambulizi hayo hivyo kila mmoja mwenye ndugu, familia na marafiki wawe macho.

Jeshi la Kenya limesema litashambulia miji hiyo ambayo inaaminika kuwa wanamgambo wa Al Shabaab wamejificha na kuawataka raia kukaa mbali na kambi za Al Shabaab.

Haijajulikana bado ni lini kutafanyika mashambulizi hayo katika miji hiyo ingawa tahadhari hiyo imetolewa.

Katika hatua nyingine hapo jana waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga alisema kuwa itasikitisha sana ikiwa raia watapoteza maisha wakati wa mapambano hayo na kuwa uchunguzi utafanyika ikiwa vifo hivyo vitatokea.

Kauli ya Odinga imekuja baada ya shirika la kimataifa la msalaba mwekundu kutoa ripoti kuwa raia wa Somalia waliathiriwa na kusema kuwa imerejea tena zoezi la ugawaji wa msaada wa chakula kwa zaidi ya watu 6000 katika kambi kusini mwa Somalia.

Jeshi la Kenya limethibitisha kuwa lilitekeleza shambulio la anga lakini jeshi hilo limepeleka lawama kwa wapiganaji wa somalia kwa kusababisha vifo.