NIGERIA

Boko Haram yapinga operesheni ya wananchi kunyang'anywa silaha na polisi

Polisi wakikagua moja ya gari katika mji wa Maiduguri
Polisi wakikagua moja ya gari katika mji wa Maiduguri REUTERS/Afolabi Sotunde

Siku moja baada ya Jeshi la Polisi nchini Nigeria kuanza msako wa silaha unaendeshwa kwa mtindo wa nyumba kwa nyumba katika Jiji la Maiduguri kundi la Waislam wenye Msimamo Mkali la Boko Haram limepinga zoezi hilo.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Kundi la Boko Haram Abu Qaqa amewaambia wanahabari wanapinga mpango huo na kuchukua nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Maiduguri kutokubali kuporwa uhuru wao kwani huenda maadui zao wakaja kuwashambulia wakishanyang'anywa silaha zao.

Qaqa ambaye mara kadhaa amekuwa akitolea ufafanuzi na misimamo maamuzi ya Kundi la Boko Haram amesema kuwa silaha walizonazo wakazi hao ndiyo ulinzi wako pekee na iwapo zitachukuliwa ni wazi watakuwa kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa.

Polisi nchini humo kupitia kwa mkuu wa operesheni ya kijeshi katika mji huo ilitangaza kuanza msako wa nyumba kwa nyumba ili kuwasaka wanamgambo wa Boko Haram ambao wanatuhumiwa kuficha silaha zao kwenye nyumba za raia na baadae kufanya nazo uasi.

Kundi la Boko Haram limekuwa likiendesha mashambulizi yakushutukiza katika Mji wa Maiduguri hali iliyoifanya serikali ya Nigeria kuamua kutangaza operesheni kali dhidi ya wafuasi wa kundi hilo