THE HEAGUE-LIBYA

Mahakama ya ICC yasema bado inafanya mazungumzo na mtoto wa Gaddafi kuhusu kujisalimisha kwenye mahakama hiyo

Seif al-Islam Gaddadi
Seif al-Islam Gaddadi REUTERS / Paul Hackett

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ICC Luis Moreno Ocampo amesema Mahakama yake bado inaendelea kufanya mazungumzo juu kujisalimisha kwa mtoto wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi, Seif Al Islam.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya ICC imekumbana na maswali kutoka kwa wawakilishi wa Seif Al Islam juu ya masharti ya kisheria yanayokwenda sambamba na maamuzi yake ya kujisalimisha,huku mahakama ikijibu kuwa anaweza kuwataka majaji kutomuamuru kurudi libya baada ya hukumu yeyote,halikadhalika majaji wanaweza kuamua Seif kushtakiwa nchi nyingine yeyote.

Ocampo ameonesha hofu kuwa wanajeshi wa kukodi wamekuwa wakijaribu kumsaidia mtoto Seif kutoroka.na kuongeza kuwa inawezekana serikali ya mpya ya Libya ikapewa nguvu ya kufanya maamuzi juu kesi dhidi ya Seif na ndugu wa karibu wa Gadafi na aliyekuwa mkuu wa maswala ya intelijensia Abdullah Al Senusi.

Mahakama ya ICC ilitoa waranti tarehe 27 mwezi juni dhidi ya Gadafi,Seif,na Senussi wakishutumiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binaadam wakati wa machafuko yaliyotokea nchini Libya,wakati wa maandamano ya kuuanguha utawala wa kanali Moamar Gadafi.

Mashtaka dhidi ya gadafi huenda yakafutwa baada ya mahakama kupata uthibitisho maalum juu ya kuuawa kwa gadafi tarehe 20 mwezi uliopita,huku Seif na Senusi wakiwa hawajulikani walipo.

Hata hivyo Ocampo amesema ofisi yake inafanya juhudi ili kuwaleta mbele ya mkono wa sheria.