SUDAN

Jeshi la Sudan latangaza kuuweka kwenye himaya yake mji wa Kurmuk

Kiongozi wa kundi la waasi wa Sudan Malik Agar
Kiongozi wa kundi la waasi wa Sudan Malik Agar Reuters

Jeshi la Sudan limefanikiwa kuweka kwenye himaya yake kambi imara ya waasi iliyopo Kurmuk mji ambao unatajwa kuwa na machafuko ukipatikana karibu na Blue Nile serikali na waasi wenyewe wamethibitisha kupitia taarifa zao.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Ulinzi ya Sudan imethibitsha kutokea kwa mapambano makali ambayo yamefanikisha jeshi lao kuiteka ngome ya waasi hatua ambayo imewaongezea nguvu ya kuweza kumaliza makundi kama hayo.

Mapema siku ya jumatano Rais Omar Hassan Al Bashir alitoa ahadi ya kuhakikisha jeshi lake linauchukua mji huo ili wananchi waweze kusali sarat Eid Al Adha wakiwa na amani tofauti na hofu ya kushambuliwa waliyokuwa nayo.

Hata hivyo kumezuka hofu ya kutokea machafuko kwenye mji huo ulioko mpakani kabisa na nchi Sudan Kusini ambayo imedai mara kadhaa kuwa wanajeshi wa Sudan wamekuwa wakivuka mpaka kuingia nchini humo.

Eneo la Kurmuk lilikuwa ni ngome kubwa ya waasi wanaopigana na serikali ya Sudan ambapo msemaji wa jeshi la nchi hiyo amevipongeza vikosi vyake na kueleza kuwa huo ni ushindi dhidi ya wanajeshi walioasi serikali.