DAMATURU-ABUJA

Kundi la Boko Haram latishia kufanya mashambulizi zaidi

Ramani ya maeneo mashambulizi yalipotokea
Ramani ya maeneo mashambulizi yalipotokea Reuters

Kundi la kiislam lenye msimamo mkali, Boko Haram, limetishia kutekeleza mashambulizi zaidi nchini Nigeria, baada ya shambulio la juma lililopita la vitendo vya kujitoa muhanga vilivyo sababisha vifo vya watu zaidi ya miamoja kaskazini mwa Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo , limejigamba kuhusika na matukio ya mwishoni mwa juma katika jimbo la Damaturu mji mkuu wa Yobe.

Msemaji wa Boko Haram, Abdul Qada amesema kwamba mashambulizi yaliyotokea ni madogo, yaliosalia yatakuwa makubwa zaidi hayajawahi kutokea,, na wataendelea kushambulia hadi pale serikali itakapositisha vitisho na vitimbi dhidi ya wafuasi wa kundi hilo.

 

Balozi wa Marekani nchini Nigeria amewatolea mwito raia wa Marekani wanaozuru nchini humo, kuwa waangalifu zaidi, kwani mashambulizi ya Boko Haram huenda yakalenga hoteli za kifahari za mjini Abuja.