AFRIKA KUSINI

Kiongozi wa vijana ndani ya ANC Julius Malema afungiwa kushiriki shughuli za kisiasa kwa Miaka Mitano

Aliyekuwa kiongozi wa vijana ndani ya ANC, Julius Malema
Aliyekuwa kiongozi wa vijana ndani ya ANC, Julius Malema REUTERS/Siphiwe Sibeko/Files

Chama tawala nchini Afrika kusini, ANC kimemsimamisha kushiriki shughuli za chama hicho, kiongozi wa vijana chini ya ANC ,Julius Malema kwa miaka mitano kwa Makosa ya kukigawa Chama hicho.

Matangazo ya kibiashara

Malema ambaye hakuhudhuria kusikiliza hukumu yake,amekutwa na hatia juu ya shutma tatu kati ya nne zilizokuwa zikimkabili,amevuliwa wadhifa wake wa kiongozi wa vijana wa ANC.

Uamuzi huo unamaana kuwa Malema mwenye umri wa miaka 30 hatakuwa tena kiongozi wa vijana baada ya kutumikia marufuku hiyo ya miaka mitano, isipokuwa pale tu rufaa itakapompunguzia miaka ya marufuku hiyo.

Malema alikuwa kiongozi wa vijana miaka mitatu iliyopita na kuibuka kuwa mshirika wa karibu wa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma aliyeshinda kura za urais mwaka 2009.

Baadae Malema alianza kuzikosoa siasa za Zuma na na kumsifu aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Thabo Mbeki akimsifu kuwa kiongozi bora zaidi kuliko Zuma hatua iliyomfanya kushtakiwa.

Mbali na hilo,Malema alistakiwa kwa makosa ya kuchochea kufanyika kwa mabadiliko ya utawala nchini Botswana.