SUDAN

Uhusiano wa Sudan na Sudan Kusini katika hatihati

Reuters/ Mohamed Nureldin Abdallah

Uhusiano kati ya Sudan na Jamahuri ya Sudan Kusini uko katika hli ngumu kutoakana na mapigano yanayozidi kutokea katika mipaka ya matifa hayo mawili, huku serikali ya Khartoum na ile ya Juba zikilaumiana.

Matangazo ya kibiashara

Wachambuzi wa maswala ya Sudan wanaona kuwa, machafuko hayo ambayo yametokea katika majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini na kusababisha mauji ya mamia ya watu kwa kipindi cha majumakadhaa yaliyopita.

Mapigano hayo yanaweza kuweka mazungumzo muhimu kuhusu mipaka kuwa katika hatihati, kama hatua madhubuti hazitachukuliwa na pande hizo mbili kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa.

Aidha,mpango wa kundi la waasi nchini Sudan kuendesha vuguvugu la kutaka kumwondoa rais Omar -Al-Bashir unaweza tu kufaulu ikiwa utapata uungwaji mkono na Sudan Kusini.

Jumuiya ya kimataifa inawajibika moja kwa moja katika kushughulikia mgogoro huo wa nchi hizo mbili ambazo zilitengana baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake Julai 9, mwaka 2011.