BURKINA FASO

Burkina Faso, Niger zahofia silaha za Libya

REUTERS/Ismail Zitouny

Burkinafaso na Niger zimeguswa na hali ya kutetereka kwa usalama kutokana na mgogoro wa Libya ambao wanahofia kuwa mgogoro huo umesababisha kuwepo kwa vitendo vya usafirishaji wa silaha.

Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Niger, Rafini Briji amesema hivi sasa usafirishaji wa silaha ni tishio kwa hali ya usalama katika ukanda wa magharibi mwa Afrika.

Briji amesema Niger na Burkinafaso zina wasiwasi juu ya makundi ya watu wenye silaha katika nchi zao hivyo kuondokana na tatizo hilo wameamua kuungana ili kuhakikisha usalama unaimarika.

Tangu kuanguka na kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi kumekuwa na hali ya wasi wasi kuwa silaha nyingi hivi sasa zinaweza kuwa mikononi mwa kundi la Al Qaeda huko Afrika kaskazini.

Hata hivyo serikali ya mpito ya Libya imeahidi kuhakikisha silaha zote zilizoko katika mikono ya raia ili kuepusha hali ya machafuko na wasiwasi kuhusu hali ya usalama.