Swaziland

Swaziland yapata mkopo kutoka benki za ndani kulipa mishahara

/AFP PABALLO THEKISO

Swaziland imefanikiwa kupata mkopo kutoka kwa benki za nchini humo na wafanyabiashara ili kulipa mishahara ya wafanyakazi wa serikali katika muda mwafaka mwezi huu.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limekuja baada ya kuwepo na uchangiaji wa fedha wa dharura wa dola za Marekani milioni 43 kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi wa umma.

Wafanyakazi wa serikali walitishia kufanya maandamano mapya baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa hundi za malipo zitachelewa kwa wiki mbili.

Serikali ya nchi hiyo imekataa kuweka wazi namna mikopo hiyo ilivyotolewa, ikiwemo viwango vya riba, hali kadhalika haijulikani namna gani mishahara itapatikana kwa ajili ya mwezi ujao.

Serikali inataka kupunguza asilimia kumi ya mishahara ya wafanyakazi wa serikali, hatua iliyopingwa vikali na vyama vya wafanyakazi, wakimshutumu mfalme wa nchi hiyo Mswati wa 3 kwa kuishi maisha ya anasa yeye na wake zake 13.