Kenya

Kenya, Ethiopia wajipanga kupeleka majeshi Somalia, vijana Misri kupambana na picha chafu

Reuters / Luc Gnago

Viongozi wa Ethiopia na Kenya pembezoni mwa Mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika AU wanatarajia kujadili mpango wao wa kupeleka majeshi nchini Somalia kuungana na wajeshi wa kulinda amani wa Umoja huo AMISOM.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa AU Nissa Roguiai amesema kuwa mazungumzo hayo yataamua iwapo nchi hizo zipeleke majeshi yake huko Somalia ili kuongeza nguvu na kuungana na majeshi ya Uganda na Burundi yaliyopo huko.

Mkutano huo wa viongozi wa nchi za Ethiopia na Kenya utafanyika baada ya wanachama wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja huo kujadili machafuko ambayo yanayoendelea nchini Somalia yakicahangia na Kundi la Wanamgambo wa Al Shabab.

Kundi la Vijana ambalo lilisaidia mapinduzi ya kuondoa madarakani Utawala wa Rais wa Misri Hosni Mubarak kwa sasa wameanza mapambano ya kukabiliana na utumwaji wa picha za wanawake waliouchi kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimetolewa na Kundi hilo lenye ushawishi mkubwa nchini Misri limesema litahakikisha linakabiliana na tabia hiyo chafu ya utumwaji wa picha za utupu za wanawake .

Kundi hilo limeweka bayana kuwa linakerwa mno na vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na wanawake wa taifa hilo kwani haziendani kabisa na tamaduni za kidini ambazo zinaongoza nchi hiyo.