Swaziland

Swaziland yakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi

RFI

Serikali ya Swaziland imeshindwa kulipa zaidi ya dola za kimarekani milioni kumi kwa sababu ya hali ya kutetereka kwa uchumi wa taifa hilo. 

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imethibitishwa afisa mmoja kutoka shirika la fedha duniani, IMF na Serikali ya nchi hiyo ikilaumiwa kwa matumizi ya makubwa na ya anasa wakati wananchi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Serikali ya Swaziland imeshauriwa kuwa ni lazima ipunguze kiasi cha malipo ya ndani ili kupambana na tatizo la kiuchumi

Swaziland ina idadi kubwa ya watu walioathirika na virusi vya ukimwi ,na kuacha watoto yatima takriban elfu 69.

Serikali ya Mfalme Mswati III imedai kuwa matatizo yake ya kiuchumi yamechangiwa na tatizo la kuyumba kwa uchumi wa dunia na si matumizi mabaya ya serikali yake.

Katika hatua nyingine wachambuzi wa mambo wamesema kuwa matumizi ya anasa ya Mfalme Mswati III na wake zake kumi na watatu yamechangia hali mbaya ya uchumi wa taifa hilo.