Misri

Maandamano makubwa kuushinikiza utawala wa kijeshi kukabizi madaraka yafanyika Misri

MAHMUD HAMS / AFP

Maandano makubwa yaliyoitishwa na vikundi vya kiislamu na watu wenye msimamo wa wastani yanafanyika jijini Cairo nchini Misri kwa ajili ya kuushinikiza utawala wa kijeshi kukabidhi madara kwa serikali ya kiraia.

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya wananchi wa wamejitokeza katika uwanja wa Tahrir Square kwa ajili kutekeleza nia yao hiyo ya kuutaka utawala huo kukaa kando.

Maandamano kama hayo pia yamefanyika mjini Alexandria na maandamano hayo yamepewa jina la ijumaa ya kudai haki ya kuwa na utawala wa kiraia badala ya utawala wa kijeshi.

Kikundi cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa utawala wa kijeshi umejaa udikteta na kimeahidi kufanya maandamano zaidi kama hali itaendelea kuwa hivyo.

Kikundi hicho kimeitaka Serikali ya kijeshi kukabidhi madaraka haraka iwezekanavyo ili kuepusha maandamano ambayo yanaweza kuleta machafuko nchini humo.