SUDAN

Wakimbizi Sudan Kusini waandamana na kuuonya Umoja wa Mataifa

© Reuters

Mamia ya wakimbizi waliokimbia mapigano nchini Sudan Kusini wameandamana jana wakilalamika juu ya udhaifu wa Umoja wa Mataifa katika kulinda raia wa Sudan kutokana na wasiwasi wa usalama unaosababishwa na migogoro ya mara kwa mara nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Halikadhalika wakimbizi hao wamelalamikia upungufu wa misaada ya kibinaadam katika kambi ya Sudani Kusini iliyoshambuliwa kwa bomu juma lililopita.

Wakimbizi hao wamemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa macho na wameutaka Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo vya anga kuzuia jeshi la Sudan kushambulia raia wa Sudan Kusini katika eneo la Kordofan Kusini na eneo la mpaka wa nchi hiyo.

Kaimu mwenyekiti wa kambi ya wakimbizi, Mustafa Jamus ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kuwa makini kufuatilia vitendo vya uonevu dhidi ya jamii ya Wanuba kwa kile alichodai kuwa wanauawa na utawala wa Omar al Bashir.

Wakati huohuo wajumbe wanaopambana na ugaidi wamekuatana jana kujadili namna ya kuzuia vitendo vya ufadhili wa fedha kwa makundi ya wanamgambo wenye silaha, hasa wakilenga Afrika kaskazini.

Wajumbe kutoka nchi 30 wameshiriki katika mkutano huo wa siku mbili uliokuwa kwa ukidhaminiwa na Uturuki na Marekani na kufanyika Algeria na Canada.

Kundi la kigaidi la AQIM lenye wafuasi takriban 400, wamekuwa wakifanya mashambulizi vikiwemo vitendo vya utekaji nyara katika nchi za Algeria, Mali, Mauritania na Niger, huku wataalam hao wakitaka juhudi za kimataifa zisaidie katika kupambana na tatizo hilo.