Misri

Watu wawili wameuwawa katika mapambano kati ya waandamanaji na polisi nchini Misri.

REUTERS/Asmaa Waguih

Mapambano makali yamezuka nchini Misri kati ya waandamanaji na mamia ya askari polisi waliojitokeza kudhibiti maandamano hayo ambapo mtu 1 ametajwa kupoteza maisha wakati 676 wakijeruhiwa katika mji wa Cairo. 

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa usalama wamesema kuwa waandamanaji hao waliungana na kujaa nje ya jengo la makao makuu ya shirika la usalama wa bandari ya jijini Alexandria pamoja na miji ya Aswan upande wa kusini na Suez kwenye Bahari ya Shamu.

Mashahidi wa maandamano hayo wameviambia vyombo vya habari kuwa vurugu za mjini Cairo zimeanza wakati polisi wa kutuliza ghasia walipojaribu kusambaratisha waandamanaji waliokuwa wamepiga kambi kuadhimisha kumbukumbu ya vifo vya waandamanaji 200ambao waliuwawa wakiwa kambini.