CAIRO-MISRI

Hali bado tete nchini Misri licha ya wito wa kufanya mjadala wa kitaifa

Maelfu ya wananchi wa Misri wakiwa katika uwanja wa Tahrir usiku wa kuamkia leo
Maelfu ya wananchi wa Misri wakiwa katika uwanja wa Tahrir usiku wa kuamkia leo Reuters

Hali imeendelea kuwa tete nchini Misri huku wanaharakati wakiwataka wananchi kujitokeza kwa uwingi kwenye uwanja wa Tahrir kuushinikiza utawala wa kijeshi kukabidhi madaraka kwa Serikali ya kiraia.

Matangazo ya kibiashara

Kufuatia kuripotiwa vifo vya watu zaidi ya 30, baraza la mawaziri linaloongozwa na Essam Sharaf limetangaza kuandika barua kwa mkuu wa baraza la kijeshi nchini humo Mohammed Hegazy kwa nia ya kujiuzulu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo zinasema kuwa baraza hilo la mpito la mawaziri limeelezwa kuwa viongozi wake walikutana hapo jana kwa dharura kujadili hali ya machafuko yanayoendelea nchini humo ambapo kwa pamoja waliazimia kuandika barua kwa baraza la kijeshi kueleza nia yao ya kujiuzulu.

Hata hivyo mkuu wa baraza la kijeshi nchini humo hajazungumzia lolote kuhusu kujiuzulu kwa baraza la mawaziri ingawa ameendelea kusisitiza kuwa uchaguzi mkuu wa bunge utafanyika kama ulivyopangwa

Toka siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita maelfu ya wananchi waliandamana katika uwanja wa Tahrir wakishinikiza serikali ya kijeshi kukabidhi madaraka kwa Serikali ya kiraia kama waivyoahidi mara baada ya kuwangushwa kwa utawala wa rais Hosni Mubarak.

Licha ya wanaharakati kuitisha maandamano vikosi vya usalama vimeendelea kujiweka mbali na waandamanaji kwa lengo la kuzuia vifo zaidi.

Madaktari katika hospitali mbalimbali nchini humo wameripoti kupokea majeruhi wanaotokana na kujeruhiwa kwa risasi na mabomu na kuongeza kuwa huenda idadi ya watu waliokufa kutokana na machafuko hayo yakaongezek.